Thursday, 25 July 2019
USAWA WA KIJINSIA TANZANIA
Usawa wa kijinsia ni lengo la jitihada za kuleta usawa kati ya jinsia zote, kutokana na dhuluma mbalimbali za jinsia moja dhidi ya nyingine.
Usawa wa kijinsia unahusiana na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na maendeleo ya kiuchumi. UNICEF inafafanua usawa wa kijinsia kama "kusawazisha uwanja wa kucheza kwa wasichana na wanawake kwa kuhakikisha kwamba watoto wote wana fursa sawa ya kuendeleza vipaji vyao".
Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (United Nations Population Fund) ulitangaza usawa wa kijinsia "kwanza kabisa kama haki ya binadamu".
Usawa wa kijinsia ni mojawapo kati ya malengo ya "mradi wa Milenia" wa Umoja wa Mataifa unaotarajia kumaliza umaskini ulimwenguni ufikapo mwaka 2015; mradi huo unadai, "Kila lengo linahusiana moja kwa moja na haki za wanawake, na jamii ambamo wanawake hawana haki kama za wanaume kamwe haziwezi kufanikisha maendeleo kwa namna endelevu".
Hivyo, kukuza usawa wa kijinsia kunaonekana kama himizo kwa mafanikio makubwa ya uchumi. Kwa mfano, mataifa ya Kiarabu ambayo yanawanyima wanawake usawa yalionywa katika ripoti iliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2008 kwamba kitendo cha kuwanyima mamlaka wanawake ni kipengele muhimu kinachodhalilisha kurudi kwa mataifa haya katika nafasi ya kwanza ya uongozi wa dunia katika biashara, elimu na utamaduni.
Monday, 22 July 2019
ATHARI ZA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Kutokana na ongezeko la ukatili dhidi ya watoto katika nchi nyingi barani Afrika, nchini Tanzania , mashirika zaidi ya 40 yamekutana kutafuta mbinu za kukomesha udhalilishaji wa watoto nchini Tanzania.
Hatua hii inakuja wakati ambapo kuna ongezeko la watumiaji wa mitandao na watoto wakiwa miongoni mwao.
Katika kizazi cha sasa ambapo unakuta teknolojia imekuwa , si jambo la ajabu kukuta picha ya mtoto kwenye mitandao bila ridhaa yake.
Dr.Herzon Zakaria Onditi,mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es salaam amefanya utafiti juu ya unyanyasaji wa kwenye mitandao na kubaini kuwa si watoto wa Tanzania pekee wanaoathirika bali ni tatizo linaloikabili dunia kwa ujumla.
Takribani asilimia 42 ya watoto ambao ni sawa na watoto wanne kati ya kumi, wameonyesha kuwa wamewahi kuwanyanyasa wenzao kwenye mtandao.
Walifanya hivyo kwa kuwatumia ujumbe wa kuudhi au picha ambazo hazina staha.Na hao wanaofanya vitendo hivyo ni wale wanaowafahamu na wakati mwingine hawawafahamu.
Asilimia 60 ya watoto wameripoti kunyanyaswa katika mtandao
Sunday, 21 July 2019
UKATILI WA KINSIA TANZANIA
Tanzania imekuwa ikitumia kauli mbiu ya "Funguka! Usalama wake, Wajibu wangu!" katika kujaribu kuongeza hamasa dhidi ya ukatili wa kijinsia mwaka huu.
Katika Haba na Haba dunia inapomaliza siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia tunakuuliza, unachukua hatua gani kupunguza ukatili wa jinsia Tanzania?
Friday, 19 July 2019
FAHAMU KUHUSU JINSIA
Jinsia ni hali ya viumbe hai wengi kuwa wa kiume au wa kike, jambo muhimu katika mpango wa kuendeleza uhai kupitia uzazi. Hata hivyo, si viumbe vyote vinaendeleza uhai kwa njia ya uzaliano kijinsia:
viumbehai vya mfuto kama bakteria vyenye mwili wa seli moja tu vinatumia uzaliano peke ambako seli hujigawa.
mimea kadhaa huzaa kwa kutenga tu sehemu ya mizizi inayoanzisha mmea mpya; mbinu hiyohiyo hufuatwa kwa kutumia kipandikizi cha kupanda katika kilimo.
mimea kadhaa huzaa kwa kutenga tu sehemu ya mizizi inayoanzisha mmea mpya; mbinu hiyohiyo hufuatwa kwa kutumia kipandikizi cha kupanda katika kilimo.
Kuna pia njia ya kujizalisha ambayo ni namna ya pekee ya uzalioni kijinsia. Mimea kama karanga na pia wanyama kadhaa mfano vyawa na samaki kadhaa wanaweza kuanzisha wadogo bila manii ya kiume. Wanyama kama mategu ni huntha wanaobeba manii pamoja na vijiyai mwilini na wanazaa ndani yao.
Subscribe to:
Posts (Atom)