Friday, 19 July 2019

FAHAMU KUHUSU JINSIA

Jinsia ni hali ya viumbe hai wengi kuwa wa kiume au wa kike, jambo muhimu katika mpango wa kuendeleza uhai kupitia uzazi. Hata hivyo, si viumbe vyote vinaendeleza uhai kwa njia ya uzaliano kijinsia:


    viumbehai vya mfuto kama bakteria vyenye mwili wa seli moja tu vinatumia uzaliano peke ambako seli hujigawa.
    mimea kadhaa huzaa kwa kutenga tu sehemu ya mizizi inayoanzisha mmea mpya; mbinu hiyohiyo hufuatwa kwa kutumia kipandikizi cha kupanda katika kilimo.
Kuna pia njia ya kujizalisha ambayo ni namna ya pekee ya uzalioni kijinsia. Mimea kama karanga na pia wanyama kadhaa mfano vyawa na samaki kadhaa wanaweza kuanzisha wadogo bila manii ya kiume. Wanyama kama mategu ni huntha wanaobeba manii pamoja na vijiyai mwilini na wanazaa ndani yao.

1 comment: