Kutokana na ongezeko la ukatili dhidi ya watoto katika nchi nyingi barani Afrika, nchini Tanzania , mashirika zaidi ya 40 yamekutana kutafuta mbinu za kukomesha udhalilishaji wa watoto nchini Tanzania.
Hatua hii inakuja wakati ambapo kuna ongezeko la watumiaji wa mitandao na watoto wakiwa miongoni mwao.
Katika kizazi cha sasa ambapo unakuta teknolojia imekuwa , si jambo la ajabu kukuta picha ya mtoto kwenye mitandao bila ridhaa yake.
Dr.Herzon Zakaria Onditi,mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es salaam amefanya utafiti juu ya unyanyasaji wa kwenye mitandao na kubaini kuwa si watoto wa Tanzania pekee wanaoathirika bali ni tatizo linaloikabili dunia kwa ujumla.
Takribani asilimia 42 ya watoto ambao ni sawa na watoto wanne kati ya kumi, wameonyesha kuwa wamewahi kuwanyanyasa wenzao kwenye mtandao.
Walifanya hivyo kwa kuwatumia ujumbe wa kuudhi au picha ambazo hazina staha.Na hao wanaofanya vitendo hivyo ni wale wanaowafahamu na wakati mwingine hawawafahamu.
Asilimia 60 ya watoto wameripoti kunyanyaswa katika mtandao
Sasa nimefahamu meeengii Sana kuhusiana na unyanyasaji na athari zake
ReplyDeleteAsante Karibu
ReplyDelete